English | Swahili  | Nederlands | Credits |

Dar es Salaam kwa Delft Blue

Utangulizi

Mwishoni mwa mwaka 1998 nilikaa kwa miezi mitatu Dar es Salaam, Tanzania, nikifundisha kupiga picha katika taasisi mojawapo. Katika kipindi hicho nilikumbana na tofauti kubwa kati ya utamaduni wa kitanzania na wangu wa kidachi. Kwa bahati mbaya, tofauti hizi za kitamaduni zinasababisha kutoelewana kirahisi.

Hata hivyo, baada ya miezi mitatu, nimegundua kwamba tofauti hizi zinaweza kutatuliwa na kueleweka. Kwa muongozo, uvumilivu na moyo wa ujasiri wa baadhi ya watanzania walionionyesha utamaduni wao, niligundua kwamba sote tu sawa, licha ya tabaka za rangi, makazi na mengineyo. Ni mazingira tunayoishi ambayo huleta tofauti kama hizi.

Ni katika kuelewa yote hayo, niliwaomba jirani zangu na watu wengine niwapige picha na vitu wavipendavyo. Kila mmoja nilimuuliza ni kwa nini amechagua kupiga picha na kitu hicho.
Baadhi ya picha hizo zinaonyeshwa hapa kwa ajili ya wale wenye nia ya kujifunza na kuelewa juu ya maisha, ikiwa wanaweza kuutumia mtandao huu wa internet.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wote walionisaidia, hasa Andrew, Sandile, Mary na Bwana mzee Sir John.

Barend Schweigman
Dar es Salaam /
Amsterdam,
Desemba 1999